F3 KISW OPENER TERM 3 2026
Document Details
Document Preview
Word Editable SampleKISWAHILI KIDATO CHA TATU
MUHULA WA TATU 2026
MUDA: SAA 2
JINA………………………………NAMBARI YA USAJILI………………………
TAREHE………………………...SAHIHI……………………………………….
1UFAHAMU(Alama 15)
Soma kifungu kifuatacho kisha ujibu maswali.
Siku hiyo Bi. Nyangweso aliwasili nyumbani muda mfupi kabla alama ya saa kugonga majira ya saa sita usiku kamili. Alitazama nyumba yake ilivyopangwa vizuri, kila kitu kimekaa mahali pake. Mandhari haya yaliufanya moyo wake kutua na tabasamu kubwa kumvaa. Mezani alitazama akaona vitabu vya mwanawe vimepangwa vizuri vikisubiri arauke na kuvitwaa kwenda shuleni. Aliridhika na kujihisi mwepesi mithili ya mtu aliyeutua mzigo mzito aliokuwa kabebeshwa masafa marefu.
Bi. Nyangweso alikuwa mteja maarufu wa mashirika mengi ya ndege yaliyompa huduma aliyohitaji. Alisafiri mara kwa mara ndani na nje ya nchi kwa ajili ya ajira yake iliyohitaji uwakilishi wake. Safari hizi zilimwezesha kukutana na marafiki wapya, hali kadhalika fursa mpya zilizompa changamoto na chagizo, si neno fursa zilikuja na mafungo gani. Aliona heri kuzikumbatia na kuzitumia vizuri walau apate kuuandalia vyema mustakabali wake na wa mwanawe.
Siku hiyo ya Bi. Nyangweso kurejea ilikuwa miezi miwili kamili tangu kuondoka kwake na kwenda ng'ambo kwa sababu ya mahitaji ya kikazi. Alikuwa amekipeza kitoto chake, na leo aliporudi tayari kilikuwa kimelala kitambo. Fikra zilimcheza shere na kumfanya kuduwaa. Upande mmoja ulimnasihi akiamshe huku mwingine ukimsimanga na kumsuta. Aliona heri akiamshe na wakati huo huo akaona atakidhulumu kwa kukikatizia usingizi. Kwa kuwa siku iliyofuata ilikuwa siku ya kwenda skuli, aliona afadhali akiachie usingizi wacho na kurauka nacho kinapojiandaa kwenda skuli. Basi aliingia chumbani mwake akayakung'uta mablanketi yake kabla ya kukiachia kichwa chake kuudara mto.
Asubuhi ile alipoamka Bi. Nyangweso alikuta jua linakaribia kulingana. Mwanga wake ulikuwa umezagaa mwote chumbani kumfanya ashindwe kuona vizuri. Alishangaa jinsi usingizi ulivyomtwaa na kumfanya kupitiliwa kiasi kile. Hatimaye aliamka taratibu na kuelekea sebuleni ambapo alimkuta msichana wa kazi ametulia baada ya hekaheka za kupunguza kazi pale nyumbani. Mazungumzo yalipotamatisha kipindi cha salamu, Bi. Nyangweso alitaka kupata habari kuhusu mwanawe.
"Tuma, mwanangu vipi?"
"Hana neno ila siku moja alikuwa na joto jingi nikampeleka hospitali kupata dawa."
"Aah!" alimaka Bi. Nyangweso. "Iweje Tuma kwamba mwanangu, hili jicho moja, awe ameugua kiasi hicho wala usinidokezee katika mazungumzo yetu?"
"Si hivyo eti. Mimi niliona nitakuchanganya kukupa habari hizo. Mwenyewe umekuwa huko ughaibuni na shughuli zote hizo halafu nikuongeze na mengine? La hasha! Halikuwa kubwa la kukuhitaji wewe kuwepo wala kujua."
Bi. Nyangweso aliyatia maneno yale katika mizani. Aliyaona yenye ukweli mtupu. Alijua kuwa kazi zile alizopenda kujitolea kufanya zilikuwa taratibu zinamtenga na mwanawe. Japo alishukuru kuwa alikuwa na mtu mwema wa kumwangalizia mwanawe, alimwonea wivu. Alianza kutambua kuwa Tuma alikuwa amechukua nafasi yake kama mzazi bila kumnyang'anya. Aliona kuwa mwanawe anakua bila yeye kuwa shahidi wa ukuaji wake. Mara ngapi amefanya kazi za shuleni na mwanawe kupitia skype? Mtandao uliwaunganisha vizuri wakazungumza karibu kila jioni kabla ya kuiaga siku, kwa hisani ya Tuma. Alikuwa akifurahi sana na kujihongera kwa mawasiliano na mwongozo wa kila siku kwa njia ya mtandao. Hata hivyo, sasa alianza kuona kuwa lilikuwepo pengo kubwa baina yake na mwanawe. Alijihisi mtupu moyoni. Alianza kuona mizani yake ya maisha ikielemea upande ambao hakuukusudia tangu hapo. Machozi yalimlengalenga naye akawa anafanya vita kuyazuia yasije yakamwagika mbele ya mwajiriwa wake.
This document is professionally prepared and verified for Form 3 (Secondary (8-4-4)) • Term 3.
- Competency-driven teacher inquiry models
- Guiding questions for active learner engagement
- Real-life problem-solving applications
- Formative & summative assessment indicators
- Performance levels (Exceeding, Meeting, Approaching)
- Practical assessment task breakdowns